ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Tuesday, January 6, 2015

SIMBA KUMCHANGIA ALEX

Wachezaji wa Simba ambao walishiriki katika kikosi kilichoing’oa Zamalek mwaka 2003 wameamua kumchangia mwenzao Christoper Alex Massawe.


Massawe yu mgonjwa taabani kwao Dodoma. Hali ambayo imewafanya Simba walioifunga Zamalek, Massawe akifunga penalti ya mwisho iliyoihakikishia Simba ushindi.

Kiungo huyo anaumwa na imeelezwa anasumbuliwa na kifua kikuu ingawa bado jambo hilo halijatolewa ufafanuzi na familia yake.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Boniface Pawasa ambaye alicheza namba tano katika mechi hiyo amesema wanaandaa mechi ya kirafiki.

“Lengo ni kupata mechi ambayo itamsaidia ndugu yetu kupata matibabu.

“Wikiendi hii tunaweza kucheza pale Karume kama hakutakuwa na mechi ya daraja la kwanza. Hili ni jukumu letu, wadau wajitokeze.


“Tayari baadhi ya waliocheza siku hiyo wamejitokeza, Emmanuel Gabriel na Victor Costa tumeishakubaliana," alisema.
Imehamishwa toka kwa Saleh Ally

No comments:

Post a Comment