ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Wednesday, January 7, 2015

LENGO NI UBINGWA WA LIGI KUU TANZANIA BARA


Zanzibar
Kocha mpya wa Simba, Goran Kopunivic amesema Ligi kuu Bara ni muhimu zaidi kwao, lakini wanataka kushinda zaidi katika mechi za Kombe la Mapinduzi.


Kopunovic amesema, amezungumza na wachezaji wake na kuwaambia ni muhimu kushinda mechi ya leo dhidi ya Taifa ya Jang’ombe.

“Wanajua tunatakiwa kushinda, ni muhimu sana kwa kuwa ni mechi ya mashindano yanayoheshimika. Lakini hii ni sehemu ya maandalizi yetu ya ligi.

“Tukishinda mechi ya leo (dhidi ya Jang’ombe), maana yake tunapata nafasi ya kusonga mbele na tunaweza kupata nafasi nyingine ya kuendelea kujiandaa.

“Hivyo ni vizuri kushinda kila mechi ya Mapinduzi ili kujiimarisha kwa ajili ya ligi,” alisema Kopunovic dakika chache kabla ya mechi kati ya Simba dhidi ya Taifa Jang’ombe.


Mechi hiyo ya robo fainali ya Kombe la Mapinduzi inaendelea kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa.

No comments:

Post a Comment