ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Friday, February 6, 2015

OKWI AONDOKA NA AGGREY MORRIS, MAGULI AONDOKA NA NYOSSO



TFF imeamka sasa baada ya kuamua kumfungia kitasa wa Mbeya City, Juma Said Nyosso.


Nyosso atakaa nje kwa mechi nane kwa kosa la kumdhalilisha mshambuliaji wa Simba SC, Elius Maguri timu hizo zilipokutana Januari 28, mwaka huu.

Pamoja na Nyosso, beki wa Azam FC, Aggrey Morris naye amefungiwa mechi tatu kutokana na lile sakata la kumpiga kiwiko mshambuliaji Emmanuel Okwi wa Simba.


Morris amefungiwa mechi tatu baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga kwa makusudi kisukusuku mshambuliaji wa SImba SC, Emmnauel Okwi timu hizo zilipokutana Januari 25, mwaka huu.

Okwi alipoteza fahamu baada ya kupigwa na Aggrey na kulazimika kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Taifa, Muhimbili, Dar es Salaam kwa matibabu zaidi na taarifa za Madaktari zilisema Mganda huyo angeweza kupoteza uhai siku hiyo kama si kuwahiwa kwa huduma ya kwanza. 

Mechi zote hizo zilifanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba SC ikitoa sare ya 1-1 na Azam FC kabla ya kufungwa 2-1 na Mbeya City.

Katika kikao chake cha awali, Februari 3, mwaka huu Kamati hiyo ya Nidhamu ilitoa adhabu kwa watu tisa wakiwemo viongozi, wachezaji na kocha mmoja kwa kupatikana na hatia ya makosa ya kinidhamu.

Okwi alilazimika kukimbizwa hospitali baada ya kuanguka na kupoteza fahamu na baadaye mikanda ya Azam TV ilionyesha Morris akimpiga.

Kwa upande wa Nyosso, amebainika amefanya hivyo baada ya picha zilizopigwa na gazeti namba moja la michezo nchini kumnasa akifanya vitendo hivyo vya kipuuzi.

Lakini tayari Nyosso ameomba msamaha kwa Maguri na Blog hii ilizungumza na wote wawili lakini Maguri akasisitiza nanachotaka ni sheria kufuata mkondo wake.

06Feb
2015

No comments:

Post a Comment