ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, September 26, 2013

JONAS MKUDE,ANAENDELEA VIZURI

Mchezaji Jonas Mkude anaendelea vizuri baaada ya kupata maumivu wakati akiitumikia timu yake ya Simba kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Ndanda fc jioni ya leo.
Akiongea na mtandao huu, Jonas alisema kuwa maumivu aliyokuwa anayasikia awali sasa hivi yamepungua kulinganisha na muda aliopata maumivu hayo.
Mechi hiyo iliyopigwa katika uwanja wa kinesi, ilishuhudia Simba Sc ikilamba mchanga baada ya kufungwa goli moja bila majibu na Ndanda fc, Simba SC leo iliwatumia wachezaji wake ambao huwa wanakosa nafasi katika michuano ya ligi kuu inayoendelea Tanzania bara huku ikiwatumia wachezaji wawili tu ambao huwa wanapata nafasi katika kiokosi cha Simba cha wachezaji waliojihakikishia nafasi katika michuano ya ligi kuu Tanzania bara
Wachezaji ambao huwa wanapata nafasi katika michuano ya ligi kuu Tanzania bara ambao walikuwepo leo hii na kupata majeraha ni Jonas Mkude na Idrissa Rashid (Baba ubaya)

No comments:

Post a Comment