ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, September 26, 2013

Ramadhani Kiparamoto ni bunduki iliyokwisha risasi Simba SC?

Ukiangalia picha kwa makini hapo juu utamuona jamaa kakaa chini bila kukalishwa, ndio amekaa tena vizuri tu ila bila kupenda.
Pembeni utamuona kijana mdogo sana akiwa katika fomu ya ajabu sana msimu mmoja uliopita, hapo ilikuwa Zanzibar katika michuano ya kombe la mapinduzi, ilikuwa mechi dhidi ya Azam Fc ambayo wachezaji wa Azam waliomba iishe mapema akiwemo captain wao wa kipindi hicho ambaye anaonekana kakaa bila kupenda Aggrey Moriss, huyu ndiye Ramadhan Kiparamoto.
Katika kumbukumbu ya kikosi bora kabisa cha vijana wenye vipaji chini ya kocha Matola huwezi kuona limekosa jina la huyu kijana, ana mashuti makali,ana pumzi na ana mwili unaokubalika yaana mwili wa kimichezo, baada ya kupandishwa kutoka Simba B kwenda Simba A inaonekana kabisa kama zama za Kiparamoto zimekwisha, je ni sahihi kusema kweli zama zake zimekwisha au ni mfumo wa kocha mpya ambaye yupo naye hivi sasa haumruhusu kufanya kazi? kwa kipindi hiki kila mtu anasema yake kuhusu kinda hili, wapo wanaosema kuwa baada ya mafanikio ya muda mfupi kaanza kujiona staa kiasi cha kwamba hata mazoezini anachelewa, pia wapo wanaosema mfumo wa mwalimu hauendani na jinsi mchezaji alivyo, sisi hatuwezi kujua tatizo ni lipi ila kwa sasa inabidi kijana aendelee na mazoezi, uvumilivu kwa kuwa yeye bado anakuwa kisoka kwani anayejua anajua tu, sitakaa kuamini kuwa kinda hili limeflop ghafla bila sababu za msingi

No comments:

Post a Comment