ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Sunday, September 29, 2013

UDHAIFU WA MASHABIKI NA WANACHAMA,NDIYO NJIA KUU INAYOTUMIWA NA VIONGOZI WETU KUTOKWENDA NA WAKATI

Hakuna shaka kabisa kuwa Simba SC ina rasilimali wanachama na mashabiki wa kutosha, hii inatokana au kwa kurithi au mapenzi ya dhat kabisa ya rasilimali hiyo kwa klabu yao.
Mashabiki ni njia mojawapo kuu kwa timu kama ya Simba Sc kujingizia kipato cha klabu,mashabiki wanaweza kuingia uwanjani au kununua bidhaa za klabu ili kuifanya klabu kuacha kuwa tegemezi sana ukilinganisha hali halisi.
Mgeni yoyote atakayetoka nja ya nchi kuja Tanzania,akiona idadi ya mashabiki wanavyojazana uwanjani,hawezi kuamini kuwa timu hiyo inategemea pesa za watu toka mifukoni na wala haiaminiki hata kukopeshwa na mabenki kwa mfumo uliopo.

Hii ni mbaya sana kwani au kwa dharau au makusudi,wanachama wanashindwa kuhoji ni kwa nini timu yetu bado ipo katika mfumo uliopo.
mfano,timu inasajili wachezaji wapya,timu inaingia mikataba na vyanzo kama vya tv au makampuni ya simu,lakini wanashindwa hata kuwaambia wanachama wao kuwa mikataba tuliyoingia gharama zake ni kiasi fulani na zinatumika kwa ajili fulani,nilitegemea timu kama ya Simba iwe na website yake ambayo wangeweka hata na vitu vya muhimu kama mikataba,mishara ya wachezaji na usajili wa wachezaji ili kupunguza maswali,kwa timu yetu imekuwa hapana.

Unapokutana na kiongozi na kumuuliza kuhusu matumizi ya klabu,jibu analikupa ni jepesi tu, 'kwani timu kambini unaiweka wewe' au kwani wewe unalipa misahara ya wachezaji?unajua tumetumia kiasi gani cha pesa katika usajili?' ni kweli sifahamu,lakini kwanini hamkutoa elimu ili kuwaelesha wanachama wenu gharama zitumikazo? mmmmh hii hapana

Timu ina afisa habari,lakini inashindwa hata kupata habari official kwani hata official page ya klabu ilishajifia zamani.

Ni bahati kwa uongozi kuwaheshimu wanachama lakini wengi wao hawajitambui,yawezekana labda wanajuana au wanashirikiana.
Wanachama sisi tunahoji tu pale tunaponyimwa tiketi za bure kwenda uwanjani,hapo ndipo tunapopaona pazuri,kuna umuhimu wa kubadilika na kujitambua.

Presha ya wanachama ikizidi kwa viongozi kwa kuwashinikiza wafanye mambo mazuri ni borz zaidi kuliko kulilia free pass au tiketi za bure viwanjani.

SIMBA NGUVU MOJA

No comments:

Post a Comment