ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, November 21, 2013

Breaking Newssss!!!! Tawi la M na Maendeleo na Wekundu wa Over waandaliwa kumpokea Rage kesho

Mwenyekiti asiyekubalika na Simba Sc ambaye amesimamishwa kikatiba na kamati ya utendaji ya Klabu hiyo Bw Ismail Aden Rage ameandaa watu kutoka matawi mawili ya Simba ya Jijini Dar Es salaam.

Habari za uhakika tulizozipata hivi punde zinasema kuwa, Lengo la kuandaa watu hao ni kuhakikisha wanakwenda a Airport kumpokea ili kucheza na akili za watu ionekane kwamba anakubalika.

Rage, alisimamishwa juzi na kamati ya utendaji ya Simba kwa kuonekana dhahiri ameshindwa kufanya kazi zake vizuri ambazo ilitakiwa afanye Huku akizembea na kuzidisha msuguano baina yake na wanachama, pia na kamati ya  utendaji.

Tawi la mpira na maendeleo maskani yake ni upanga wakati lile la Wekundu wa Over linaoatikana Kimara jijini Dar Es salaam.

No comments:

Post a Comment