ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Wednesday, November 20, 2013

Rage ilibidi aondoke ili timu ikae sawa

Jana kulikuwa na taarifa za kusimamishwa kwa mwenyekiti wa Simba Sc Ismail Aden Rage, hakika iliwashtua wanachama wengi wa Simba na Hata mashabiki pia.

Kwa wanaofatilia Simba kiundani zaidi, utagundua kulikuwa kuna ufa Kati ya wanachama, makocha na Viongozi.
Katika pande tatu hizi zilizokuwa zinapingana kisirisiri, ilikuwa hakuna jinsi zaidi ya pande mbili kuondoka ili timu iwe bora.

VIONGOZI

Hakika ni upande wenye maana kubwa kwa Klabu yetu, lakini kwa viongozi wetu hawakutuonesha Hilo, dharau za mwenyekiti wetu dhidi yetu, ujuaji wa mwenyekiti wetu, na kutotambua thamani ya wale aliyekuwa  , hakika ilitosha.
Ismail Aden Rage hakuweza kuwajua Wala kuwatambua wachezaji wa Simba Sc zaidi ya kujiweka mbele mbele timu inapofanya vizuri, kumbuka rambirambi za Mafisango , yeye Kama mwenyekiti hakujua thamani ya utu, kuingia mikataba na Azam Tv bila kumshirikisha mdau yoyote wa Simba Sc, hakika ilitosha.

Jambo pekee ambalo labda linaweza kuwa zuri ni kumuachia Mbwanna Samata akacheze Tp Mazembe tu, Kwani amensaidia mchezaji na Sio Klabu..

Ujuaji huu na uongo wake ndipo umetufikisha hapa , yapo mengi sana ila yatazidi kujulikana tu.

MAKOCHA

Kocha mkuu wa Simba Sc alipewa timu kubwa kuliko yeye, binafsi siwezi kumlaumu sana, ila kwanini alikuwa akimsikiliza sana Jamhuri Kihwelo Julio??!

Siwezi kujua ila naamini Julio Ndiye aliyeamua hatma ya Kibaden, labda walikuwa wanajua wanachofanya, matokeo yake timu ilikuwa inacheza mpira mbovu tena wa ajabu sana.

Naamini Badiliko hili la kocha mpya limekuja Muda muafaka na kwa wakati sahihi.

Simba ilikuwepo na itakuwepo, Rage iache Simba kwa Amani Kwani hautaweza tena kufanya kazi na watu wasiokuamini.

No comments:

Post a Comment