ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Friday, November 22, 2013

Simba B yaandaa mauaji ya wanajeshi wengine kesho!

Kikosi cha Simba B kesho kinatarajiwa kushuka tena katika uwanja wa Karume kukipiga na Ruvu Shooting.

Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu , inakuja baada ya KIKOSI hicho kushusha dhahama nzito kwa Wanajeshi wengine wa Mgambo.

Hapo Jana, timu hiyo inayofundishwa na nahodha wa zamani wa Simba , Selemani Matola, iliivurumisha timu ya Mgambo Jkt kwa jumla ya goli 5-0.
Shukrani kwa wachezaji Ibrahim Hajib na Issa Abdallah waliofunga Mara mbili kila mmoja, Huku Miraji Athumani akitupia msumari mmoja katika lango la Mgambo Jkt.

No comments:

Post a Comment