ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Saturday, November 30, 2013

MANENO YA JULIO HAYANA TOFAUTI NA YA MFA MAJI

Jana Jumamosi, aliyekuwa kocha wa Simba Jamhuri Kihwelo Julio, aliibuka katika vyombo mbali mbali vya habari, na kuanza kuwashambulia kwa maneno makali wanachama wawili wa Simba Sc.

Wanachama hao waliokumbwa na mkasa wa kushambuliwa na kocha huyo msaidizi wa zamani ni aliyekuwa makamo mwenyekiti wa Simba Sc kabla ya kujiuzuru mwenyewe Ndg Geodgrey Nyange Kaburu na mwenyekiti wa kamati ya ufundi ya timu hiyo Bw Ibrahim Masoud Maestro.
Julio katika maelezo yake, alidai kuwa nyuma ya yeye kusitishiwa mkataba wake wa Simba, kuna mikono ya moja kwa moja ya Ibrahim Masoud na Nyange Kaburu, huku akitoa maneno makali zaidi, Bw Julio alisema kuwa watu hao ni Sumu katika Simba, na hawafai Hata kidogo.

Ikumbukwe kuwa mkataba wa Julio na Simba Sc, ulitegemewa kuisha rasmi mwezi huu, pia ikumbukwe kuwa maneno haya ya Julio, anayatamka wakati hayupo tena ndani ya Simba, je kwanini asingetamka akiwa ndani ili watu wajue kinachoendelea ??

Binafsi namuheshimu sana Julio, pia naelewa inawezekana maneno yake yana usahihi kwa kiasi fulani, ila tatizo ni Muda alioamua kutamka maneno hayo haukuwa sahihi kabisa.
Simba ilikuwepo kabla ya Julio  Wala Kaburu, ni vizuri akatambua kuwa mwisho wa siku kamati ya utendaji ndio iliyoamua, ni vizuri atulie ili mengine yaendelee.

Siku njema.

No comments:

Post a Comment