ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, November 14, 2013

Mkude, Singano,Kiemba, Lucian, Chanongo waitwa Stars

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania , Kim Paulsen, amewaita wachezaji watano kutoka Simba ili kuwajumuisha katika kikosi kitakachoivaa Timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars.

Wachezaji walioitwa na kocha huyo ili kukiongezea nguvu kikosi chake ni viungo makinda Willium Lucian Gallas, Jonathan Gerald Mkude, Ramadhan Singano Messi, Haruna Othman Chanongo na mkongwe Amry Kiemba!


Timu hiyo ya Tanzania, itaumana na timu ya Kenya katika mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA wiki ijayo .


Wakati huo huo, Hali ya kinda lingine la Simba Abdallah Seseme inazidi kutengamaa baada ya kuumia akiwa mazoezini mwanzoni kabisa wa msimu huu

No comments:

Post a Comment