ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Monday, November 25, 2013

Simba B vs Mtibwa B robo fainali Uhai Cup

Timu ya soka ya pili ya Simba yaani Simba B, inatarajia kucheza mechi ya robo fainali dhidi ya Mtibwa Sugar hapo tarehe 28 ya mwezi huu.

Kikosi hicho kipya kinachofundishwa na nahodha wa zamani wa Simba Selemani Matola, kinatarajiwa kukutana na mtihani mgumu baada ya kupoteza mechi zake mbili za mwisho kwa watani wa goli 2-1 kila mechi.

Simba B inayotafuta nafasi ya kucheza hatua ya nusu fainali, itaongozwa na mchezaji anayekipiga katika ligi kuu Tanzania Bara Said Ndemla.

No comments:

Post a Comment