ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Sunday, February 2, 2014

SiMBA VITANI

SIMBA SC WAIFUATA MTIBWA SUGAR MAPEMAAA, LOGA ASEMA SASA ‘NGOMA INOGILE’, WATAISOMAAAA

Na Prince Akbar, Dar es Salaam
KIKOSI cha Simba kimeondoka mjini Dar es Salaam asabuhi ya leo kwenda mjini Morogoro tayari kwa ajili ya mchezo wao wa raundi ya 16 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Uwanmjja wa Jamhurio mjini humo keshokutwa Jumatano.
Kocha Msaidizi wa Simba, Suleiman Matola ameiambia BIN ZUBEIRY asubuhi hii kuwa wako ndani ya basi lao kubwa walilokabidjhiwa na wadhamini wao, Kampuni ya Bia nchini (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro kuelekea Morogoro kuwavaa mabingwa hao wa Tanzania Bara 1999 na 2000.
Sasa ngoma inogile; Kocha wa Simba SC. Zdravko Logarusic amesema washambuliaji wake sasa wanaanza kumuelewa

"Tuko ndani ya basi kwa sasa tunakwenda Morogoro kwa ajilio ya mechi inayofuata dhidi ya Mtibwa," amesema Matola ambaye alianza kuinoa Simba baada ya kutimuliwa kwa makocha Abdallah 'King' Kibadeni na msaidizi wake Jamhuri Kihwelo 'Julio' Novemba mwaka jana.
Kikosi cha Wana Msimbazi kilicho chini ya kocha Mcroatia Zdravko Logarusic, kitaingia uwanjani Jumatano kikiwa na kumbukumbu ya kuifunga Mtibwa iinayonolewa na nahodha wake wa zamani Mecky Mexime mabao 2-0 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopiggwa Uwanja wa Taifa Septemba 14 mwaka jana.
Simba inakamata nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 30 ilizozipata katika mechi 15, pointi sita nyuma ya vinara Azam FC, tano nyuma ya watani wao wa jadi, Yanga (nafasi ya pili) na moja nyuma ya Mbeya City walioko nafasi ya tatu wakati Mtibwa wako nafasi ya tano wakiwa na pointi 21. Hata hivyo, Azam FC, Yanga na Mbeya City wamecheza mechi moja zaidi ya Simba.
Mapema jana, Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic 'Loga' alitamba kuwa washambuliaji wake sasa wameanza kukamata mfumo wake wa ufundishaji wa soka baada ya kuiangamiza bila huruma mabao 4-0 timu ya 'maafande' wa Oljoro JKT inayonolewa na kocha mpya Hemed Morocco katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi.
Logarusic aliiambia BIN ZUBEIRY Dar es Salaam jana mchana kuwa amefurahishwa na matokeo hayo kwa kuwa safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na Mrundi Amisi Tambwe imeonekana kuukamata ufundishaji wake.
Amesema tangu atue Simba Desemba 2, mwaka jana kurithi mikoba ya Abdallah 'King' Kibadeni aliyetimuliwa, timu yake imekuwa ikifanya vizuri katika safu za ulinzi na kiungo lakini imekuwa ikirudiswa nyuma na safu ya ushambuliaji.
"Tumeanza mzunguko wa kwanza wa ligi kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0 (dhidi ya Rhino Rangers Januari 26), hii ni hatari maana muda wowote timu mnayocheza nayo inaweza kusawazisha na kuwagharimu kifikira. Tumelifanyia kazi suala hilo, naamini tutaendelea kushinda kwa idadi kubwa ya mabao kwa sababu wachezaji wanaonekana kushika tunachowafundisha," amesema.
"Baada ya kuanza kuifundisha Simba, jukumu la kwanza ilikuwa kuelewa uwezo wa kila mchezaji, Awadh (Juma) alikuwa anacheza kama kiungo mkabaji lakini sasa anacheza nyuma ya washambuliaji. Messi (Ramadhani Singano) alikuwa akicheza kama kiungo, sasa anacheza kama mshambuliaji.
"Kwa sasa naamini mabao mengi yatafungwa na washambuliaji kwa sababu tumezungumza na viungo na kuwaambia waache uchoyo na hilo tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa, jana (juzi) Messi alikuwa na uwezo wa kufunga mabao mawili katika pasi zake tatu za mabao matatu aliyopika, lakini hakuna sababu ya kufanya hivyo kwa kuwa washambuliaji ndiyo waliokuwa na nafasi kubwa za kufunga," amesema zaidi kocha huyo wa zamani wa mabingwa wa Kenya, Klabu ya Gor Mahia.
Mabao ya Simba katika mechi hiyo iliyoshuhudiwa na maelfu ya watazamaji akiwamo Kocha wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Kim Poulsen yalifungwa na kiungo mkabaji Jonas Mkude dakika ya 10 kabla mfungaji bora wa Kombe la Kagame na Ligi Kuu ya Burundi msimu uliopita, Amisi Tambwe hajafunga mabao matatu (hat-trick) dakika ya 22, 28 na 50 ikiwa ni hat-trick yake ya pili msimu huu.
Kabla ya mechi hiyo, Simba chini ya Logarusic ilikuwa imecheza mechi nane ambazo washambuliaji wake hawakufunga hata bao moja. Mechi hizo ni sita za mashindano ya Kombe la Mapinduzi, moja ya kirafiki waliopigwa 1-0 dhidi ya 'Wakatamiwa wa Manungu', Mtibwa Sugar na mechi ya ligi waliyoshinda 1-0 dhidi ya maafande wa Rhino Rangers kutoka Tabora. Imehamishwa Toka Bin zubery

No comments:

Post a Comment