ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, August 21, 2014

MUSOTI; SIONDOKI SIMBA SC

Beki kisiki wa kikosi cha wekundu wa msimbazi Simba SC Donald Musoti,amesema bado yupo sana ndani ya mabingwa hao wa kihistoria wa Afrika Mashariki na kati yaani CECAFA.

Akiongeea na SPS Blog, Musoti amesema kuwa yeye ni mchezaji halali wa Simba SC na ana mkataba wa mwaka mmoja zaidi ." N kweli nimesikia habari za mimi kuhama ndani ya Simba SC, lakini lazima waelewe mimi nina mkataba na klabu yangu ambao hauniruhusu kuhama mpaka kwa ruhusa yao, ndio maana nipo nao hapa Zanzibar ili kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara" aliongeza beki hiyo.


Donald Musoti alijiunga na Simba SC akitokea Gormahia ya Kenya likiwa ni zao la kocha aliyekatishiwa mkataba wake Zdravko Logarusic.

No comments:

Post a Comment