ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Monday, September 29, 2014

KIONGELA AITULIZA SIMBA SC

Mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya anayechezea klabu ya Simba SC Paul Mode Kiongela amesema kuwa Simba SC ipo kamili ingawa ilisuasua katika ligi kwa mechi mbili zilizopita.

Akiongea na SPS blog, mshambuliaji huyo mwenye nguvu na aliye majeruhi kwa sasa, amesema kuwa Simba ina kikosi kipana ila anawashangaa wanasimba kuwakatisha tamaa wachezaji wao."ni kweli tunasuasua ,ila tuko wengi wenye uwezo wa hali ya juu,ni muda wa mashabiki kufahamu nini maana ya soka" aliongeza mshambuliaji huyo.

Paul Kiongela aliumizwa vibaya na kipa wa Coastal Union Shaaban Kado,katika sare ya 2-2 hali itakayopelekea mchezaji huyo akose mechi dhidi ya Yanga.

Wakat huo huo, kikosi hicho cha mitaa ya msimbazi,kinatarajiwa kuendelea na program zake za mazoezi katika uwanja wa Boko veterani jioni ya leo.

No comments:

Post a Comment