ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Sunday, September 28, 2014

PHIRI APANGUA JESHI LAKE TENA,MANICHE ATAJWA

Kocha wa timu ya Simba SC amesema kuwa huenda akaufumua mfumo aliotumia dhidi ya Polisi Morogoro ili aweze kupata pointi tatu muhimu katika mechi inayofuatia.

Akiongea na SPS blog kwa njia ya simu ,kocha huyo asiye na makeke amesema kuwa Simba SC ni timu kubwa na ina mashabiki wengi hivyo ni muhimu kuangalia jitihada zipi ili aweze kufanya vizuri.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya kikosi hicho kilichoanza ligi kwa kusuasua kulazimishwa sare ya goli 1-1 dhidi ya polisi ya Morogoro.

Bao pekee la mshambulaji wa zamani wa Simba SC Danny Mrwanda,lilitosha kabisa kuzima ndoto za wekundu hao wa Tanzania kuondoka na pointi 3 katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Wakati huo huo..baadho ya mashabiki wa Simba SC wamemtaja kuwa kukosekana kwa Awadh Juma(Maniche) ndio kunapelekea matokeo mabovu.
 
Akiongea na blog hii ,shabiki mmoja wa Simba SC aliyejitambulisha kwa jina la Ramadhan Athumani,amesema kuwa Maniche ni muhimu na wala kocha asikariri" unajua Maniche ni muhimu,kumbuka mechi ya Gormahia,nani aliwapoteza wakenya kama sio huyu" aliongeza.

No comments:

Post a Comment