ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Tuesday, September 30, 2014

SIMBA SC YAHAMISHIA KAMBI DAR ES SALAAM

Kikosi cha Simba SC kimehamishia kambi jijini Dar Es Salaam ili kujiandaa na mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Stand United.

Akiongea na mtandao huu, msemaji wa klabu ya Simba SC amesema kuwa wamehamishia kambi Dar kwa kuwa ni muda mfupi kwenda na kurudi Zanzibar.

Simba SC, imeanza kwa unyonge ligi kuu Tanzania bara baada ya kulazimishwa sare mbili mfululizo.

Wakati huo huo, mabingwa hao wa kihistoria wa Afrika Mashariki na kati leo wameendelea na mazoezi katika viwanja vya chuo kikuu jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment