ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Tuesday, September 23, 2014

MKUDE AREJEA KUNDINI...KIONGELA MASWALI TATA SIMBA SC

Kiungo 'mtukutu" cha kati wa Simba SC amejiunga na wenzaka katika kambi inayoendelea visiwani Zanzibar katika kujiandaa nac mechi zinazofuata za kuwania taji la ligi kuu Tanzania bara.

Akiongea na blog hii muda mfupi baada ya kuwasili,, Jonas amesema kuwa anafahamu kazi ni ngumu ila amewataka wanasimba kutokata tamaa kufuatia matokeo ya sare dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika dimba la uwanja wa taifa.

Wakati huo huo, mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya Raphael Mode Kiongela huenda akakaa nje muda mrefu zaidi baada ya kuumizwa na kipa wa Coastal Union Shaaban Kado.

Kiongela anatarajiwa kukaa nje kwa takriban wiki tano,hali itakayopelekea kukosa pambano la watani wa jadi dhidi ya Yanga hapo oktoba 12. 


No comments:

Post a Comment