ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Sunday, September 7, 2014

PHIRI ACHEKELEA OKWI ,BANDA KUWA HURU

Kocha mkuu wa Simba Sc Patrick Phiri amesema kuwa amefurahishwa na uamuzi wa TFF kuwaruhusu wachezaji wake wawili kuchezea kikosi cha Simba SC.

Akiongea na blog hii muda mfupi uliopita,kocha huyo amesema kuwa hakuna kocha yoyote anayeweza kupinga kuwa na mchezaji kama Emanuel Okwi au Abdi Banda." Ndio nimefurahi sana,ni jambo jema kwa kikosi changu na hata mashabiki kwa ujumla" aliongeza.

Kamati ya rufaa na hadhi ya wachezaji, leo imewaidhinisha wachezaji wawili wa Simba SC Emanuel Okwo na Abdi Banda kuchezea timu ya Simba SC baada ya kushinda rufaa zao.

No comments:

Post a Comment