ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Wednesday, October 1, 2014

SIMBA PLATINUM SUPPORTERS YAANZA KUCHUKUA WANACHAMA WAPYA

Simba Platinum Supporters imeanza kutoa kadi za uanachama wa SPS kwa wanaSimba wote bila kujali itikadi za kimatawi...lengo ni kuunganisha wadau wote kuwa sehemu moja ya Simba SC.

SPS inaundwa kwa ajili ya kuonesha kwa uwazi kile ulichonacho kwa ajili ya timu yetu pendwa...ikumbukwe kuwa Simba SC inakuhitaji sana wewe kuliko wewe unavyoihitaji katika nyanja tofauti.

VIGEZO

Uwe mwanachama/mdau/mshabiki na mkereketwa wa Simba SC
Uwe na umri wa miaka kuanzia 18
Uwe na akili timamu
uwe na wadhamini wawili toka SPS TEAM

Ada ya kuingilia pamoja na kadi ni 15000/=

Pia tumeanza kuandikisha wadau mbali mbali na tunaendelea kuandikisha ili kuweza kupata kadi za Simba SC ikiwa na malengo ya kuongeza idadi ya wanachama kufikia 50000,

kwa maelezo zaidi piga 0767460011 au 0714222345

NGUVU MOJA

No comments:

Post a Comment