ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Wednesday, October 1, 2014

BANDA KUNDINI KUIVAA STAND UNITED

Beki ya kushoto ya Simba SC Abdi Banda, anarejea dimbani jumamosi hii kuivaa Stand United katika mechi ya mzunguko wa tatu wa ligi kuu Tanzania bara.

Beki huyo aliyesimamishwa na TFF kwa matatizo ya kimkataba, anarudi dimbani baada ya kukosa mechi mbili za mwanzo.

Abdi ambaye ana uwezo wa hali ya juu wa kupiga mguu wa kushoto, alikosa mechi dhidi ya Coastal Union na ya Polisi, mechi ambazo Simba SC iliambulia pointi mbili kati ya sita.

Wakati huo huo, jeshi la wekundu wa Msimbazi The REDS ya Tanzania, leo itaendelea na mazoezi katika viwanja vya chuo kikuu jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment