KAMA SHABIKI NA MWANACHANAMA WA SIMBA SPORTS CLUB MANENO HAYA YANA UKWELI NDANI YAKE??? TUTAFAKARI
Kocha Julio: kuvurunda kwa Simba kuna mkono wa mtu
KOCHA mwenye maneno mengi ambaye pia ni
shabiki mkongwe na Simba, Jamhuri Kihwelu
‘Julio’ ameshindwa kuzuia hisia zake na kudai
kwamba matokeo inayopata timu hiyo
kwenye Ligi Kuu Bara yana mkono wa mtu.
Julio, ambaye amepata mafanikio akiwa na
Simba kama mchezaji na kocha, alidai kuna
baadhi ya viongozi wajuaji wanaoingilia uhuru
wa benchi la ufundi lililoko chini ya Mzambia,
Patrick Phiri.
Ingawa Phiri amekataa kuzungumzia hilo, Julio
amesisitiza kwamba ana uzoefu na kocha
huyo kwani aliwahi kufanya naye kazi Simba
na anaelewa hali halisi huku akidai kwamba
upole wake unamgharimu katika baadhi ya
mambo.
Simba imecheza mechi mbili za Ligi dhidi ya
Coastal Union walipotoka sare ya 2-2 na
baadaye wakatoka sare nyingine ya 1-1 dhidi
ya timu iliyosajili kikosi cha bei chee Polisi
Morogoro.
Mechi zote Simba imecheza Uwanja wa Taifa
ambao ndiyo wa kisasa zaidi nchini. Phiri akijibu
tuhuma hizo kwa kifupi alisema:
“Sipangiwi timu nafanya kazi na benchi la
ufundi, lakini viongozi wa timu kubwa kama
Simba wana mambo mengi, haya matokeo ni
sehemu ya mchezo haina haja ya kupaniki.
Timu itakaa vizuri, kilichopo hapa ni viongozi
kujenga timu kwa mfumo wa ligi nzima,
kuzingatia mechi zote za msimu si kuiangalia
kuifunga Yanga pekee.”
Julio aliyeshindwa kwenye uchaguzi mkuu
uliopita wa Simba akigombea nafasi ya
Umakamu Mwenyekiti aliiambia Mwanaspoti
kwamba: “Phiri aachwe afanye kazi yake,
aamue nani acheze na nani akae benchi
asiingiliwe.
Nimefanya kazi nikiwa msaidizi wake ndani ya
Simba na tulikuwa tukikumbana na matatizo
kama hayo ya kupangiwa timu na watu
wachache. Viongozi wafanye yao na
wamuachie kocha afanye yake na si
kumuingilia kwasababu ni mpole tu, hivi ni kuharibu.”
“Phiri ni mwalimu profeshno, anajua kazi yake
na anajua ni mchezaji gani mzuri anayeweza
kucheza kwenye mchezo fulani lakini pia
anajua mchezaji yupi hayuko fiti kucheza siku
fulani.
Naamini akiachwa afanye kazi yake Simba
itabadilika,” alidai Julio ambaye kwa sasa ni
kocha wa Mwadui FC inayoshiriki Ligi Daraja la
Kwanza.
Julio alienda mbali zaidi na kudai kwamba hata
Kocha Zdravko Logarusic aliyetimuliwa hivi
karibuni ilisababishwa na kugoma kupangiwa
kikosi na baadhi ya vigogo wa Simba.
No comments:
Post a Comment