ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, October 2, 2014

ISSA RASHID TAYARI KUWAVAA STAND UNITED, MKUDE ACHEKELEA

Beki ya Simba SC iliyokuwa majeruhi Issa Rashid(Baba ubaya), ameanza mazoezi rasmi tayari kabisa kuwavaa Stand United.

Mchezaji huyo ambaye hakucheza mechi yoyote msimu huu kutokana na majeruhi,amerejea uwanjani kwa kasi tayari kabisa kuonesha kile ambacho Simba ilikikosa katika mechi mbili zilizopita.
Simba SC imeambulia pointi mbili kati ya pointi sita hali inayopelekea sintofahamu kutokana na ubora wa kikosi hicho msimu huu.

Wakati huo huo, Kiungo maridhawa cha kati cha Simba SC Jonas Gerrald Mkude amesema wanajiandaa vizuri ili kuizima Stand United katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

The Reds ya Tanzania(Simba),inatupa karata yake ya tatu dhidi ya timu hiyo inayotoka Shinyanga, katika mechi ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa pande zote.

No comments:

Post a Comment