ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, October 2, 2014

KILICHOTOKEA USIKU WA ULAYA JANA JUMATANO

undi manne tofauti. Kwa upande wa kundi D tulishuhudia mechi mbili, mojawapo ikiwa kati ya Arsenal na Galatasaray. Arsenal ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani wa Fly Emirates iliweza kuibuka na ushindi mnono wa bao 4 kwa 1 dhidi ya mabingwa  wa Uturuki. Mchezo huo ulioanza kwa kasi sana huku ukiwa na mashambulizi ya kupokezana na kushtukizana kulingana na aina ya mchezo wa timu hizo mbili, Galatassaray kupitia kiungo wake maridadi kabisa Wesley Sneijder iliweza kushambulia katika lango la Arsenal ndani ya dakika 15 za mwanzo. Lakini baadaye hali ilibadilika baada ya Danny Welbeck kuiandikia Arsenal goli la kwanza na pia goli la kwanza la Welbeck katika ligi ya mabingwa ulaya katika dakika ya 22, goli hilo lilionesha kuanza kujiamini kwa mshambuliaji huyo liliwekwa wavuni baada ya Welbeck kupokea pasi ya shukrani kutoka kwa Alexis Sanchez. Dakika nane baadaye Welbeck aliutumia uzembe wa mabeki wawili wa Galatasaray na kujitangulizia mpira kwa kichwa mpaka kwenda kutikisa nyavu za Galatasaray na kuiandikia timu ya Arsenal goli la pili. Alexis Sanchez aliyeonekan kuisumbua sana safu ya mabeki wa Galatasaray kwa kumiliki mpira na kuukokota kama ilivyo kawaida ya mchile huyo, Lakini Felipe Melo alimfanyia madhambi mchile huyo dakika ya 34 na kupata kadi ya njano kutoka kwa muamuzi. Hata hivyo madhambi yale hayakutosha kupunguza kasi maana dakika 7 baada ya kufanyiwa madhambi Sanchez alizamisha goli la tatu baada ya kuitendea haki pasi ya kiungo mjerumani Mesuit Ozil kwa kuwafinya mabeki na kutia wavuni mpira uliompita kipa Fernando Muslera. Kipindi cha kwanza kilimalizika Arsenal ikiwa mbele kwa mabao 3 kwa 0.
         Kipindi cha pili kilianza kwa mabadiliko kutoka kwa kocha Cesare Prandeli baada ya kumtoa Yekta Kurtulus na kumuingiza kiungo mwenye uzoefu mkubwa aliyewahi kuichezea Real Madrid, Hamit Altintop. Kipindi cha pili kilichoanza kwa kasi zaidi hasa kwa hawa washika bunduki wa London ambao dakika ya 52 kupitia kwa mshambuliaji wao mpya Danny Welbeck aliyewatoka mabeki wa Galatassaray na kwenda kumalizia pasi maridadi kutoka kwa Alex Chamberlain na hivyo kujiwekea “hat trick” yake ya kwanza katika maisha yake ya soka.Na hivyo kuifanya sherehe ya kutimiza miaka 18 ya Arsene Wemger ya kuifundisha klabu ya Arsenal kuwa nzuri zaidi. Uzembe mkubwa uliosababishwa na mabeki wawili wa kati wa Arsenal ulimfanya golikipa Szczesny kufanya uamuzi mgumu na kuamua kumfanyia madhambi Mshambuliaji wa Galatassaray Burak Yilmaz katika eneo hatari na kuambulia kadi nyekundu pamoja na “penati” dhidi ya Arsenal. Dakika hiyo ya 62 ilimlazimu Arsene Wenger kufanya mabadiliko na kumuingiza golikipa Ospina na kumtoa Alexis Sanchez ili kunusuru ushindi wake. Hata hivyo David Ospina hakutosha kuzuia mpira wa penati uliopigwa kwa ufundi mkubwa na kuipa Glatassaray goli la kufutia machozi lilodumu mpaka mwisho wa mechi. Mabadiliko yalifanyika katika timu hizi mbili, kwa upande wa Arsenal iliyomtoa Oxlade Chamberlain na Mesut Ozil na kuwaingiza ili Tomas Rosicky na Jack Wilshere walio wakabaji zaidi ili kupoza  mashambulizi. Kwa upande wa Galatassaray Bruma na Umut Bulut waliingia kushika nafasi ya mkongwe Pandev na Veysel Sali ili kuongeza nguvu ya ushambuliaji na kutumia nafasi ya wachezaji kumi wa Arsenal. Hata hivyo kicwa kilichopigwa na mshambuliaji Burak Yilmaz kiliweza kuokolewa na golikipa Ospina na baadaye Santi Cazorla alitumia pasi ya Jack Wilshere vizuri, lakini mabeki wa Galatassaray waliuzia mpira ule karibia na mstari. Matokeo yalimalizika Arsenal ikiwa kifua mbele kwa goli nne (4) kwa moja(1) dhidi ya Galatasaray na Welbeck kuonekana kuwa nyota wa mchezo huo.
         Matokeo mengine ni Borrusia Dortmund aliweza kuibuka na ushindi wa mabao matatu kwa bila dhidi ya Anderlecht, Atketico Madrid iliyopata ushindi wa bao 1 kwa 0 dhidi ya Juventus bao liliofugwa na Arda Turan, Malmo ilijipatia ushindi wa mabao 2 kwa 0 dhidi ya Olympiakos, Majogoo wa wingereza Liverpool Fc waliambulia kichapo cha bao 1 kwa 0 kutoka kwa wababe Fc Basel, Real Madrid wakiwa ugenini walipata ushindi wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya wenteji wao Ludogoret, Byer Leverkusen ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani iliweza kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3 kwa 1dhidi ya Benefica nao Zenit na Monaco walitoka suluhu ya bila kufungana katika uwanja wa nyumbani wa Zenit.
                       

No comments:

Post a Comment