Adam Smith ndie gwiji la maswala ya uchumi
kuwai kutokea Duniani.Kanuni na nadharia nyingi za uchumi zimetoka kwenye
kichwa cha Adam Smith.Ukiacha Adam Smith maJabali mengine ya uchumi kuwai
kutokea Duniani ni Karl Max na John M.Keynes. John M. Keynes,Karl Max na Adam
Smith kwenye uchumi ni kama pele , Maradona na Messi kwenye soka.Ni wachumi bora kuwai kutokea
Duniani.
Pamoja
na Ubora waliokua nao Karl Max na Adam Smith bado walishindwa kutueleza ni
jinsi gani mtu atafanya maamuzi magumu na maamuzi hayo yasimletee matokeo
hasi.Pamoja na Dunia kumuhesabu kuwa ni miongoni mwa watu 100 muhimu kwenye
karne ya 20 bado Keyness alishindwa kusaidia
wafanyabiashara wadogo wadogo jinsi ya kufanya uchaguzi sahihi kati ya
vitu viwili muhimu.Unaweza ukafanya jambo dogo litakalowagusa watu wengi na
Dunia ikakukumbuka daima.Mwaka 1914 Friedrich Von Wieser aligundua kanuni ya
uchumi aliyoiita ”Opportunity Cost”(gharama
nafasi). Ukiwa na vitu viwili muhimu,ukachagua kimoja na kupoteza kimoja,hiko
kimoja ulichokichagua ndio gharama nafasi (Opportunity Cost) ya kingine
ulichokipoteza.Kiufupi kanuni ya
”Opportunity Cost” inasaidia kufanya maamuzi magumu ukiwa na mahitaji ya vitu
viwili muhimu na inabidi kwa wakati huo uchague kimoja huku ukikubali kupoteza
kingine. Huyo ndio Friedrich Von Wieser kanuni yake ya “Opportunity Cost”
ikamshawishi rais wa Australia wa wakati huo Count Heinrich Von Clam Martinic
amteue kuwa waziri wa maswala ya fedha hiyo ni miaka mitatu tangu kugundua
principle pendwa ya “opportunity cost”
Wiki kama
tatu zimepita tangu simba iamue kumrudisha mshambuliaji Emmanuel Okwi.Emmanuel Okwi kipenzi cha
washabiki na viongozi wa simba.Viongozi na washabiki wa simba walikua wakiumia
sana wakimuona Okwi amevalia uzi wa njano na kijani.Viongozi wa simba wakaamua
kufanya kila njia kumrudisha kipenzi chao Okwi.Ilikua ngumu kwa simba kwasababu
kuu mbili.Kwanza OKwi alikua ana Mkataba wa Utata na Yanga lakini Ugumu zaidi
ukaja kwa simba wenyewe ambao walikua wameshafikisha idadi ya wachezaji watano
wa kigeni ambao ni mahitaji ya kanuni ya shirikisho la mpira wa miguu
Tanzania.Hapo ndipo Akili za Kaburu,Aveva na Hans pope zilipokua zinawasha.Hapo
ndipo viongozi hao walikuwa wakifanya maamuzi huku wakikumbuka hekima za mtunzi maarufu wa vitabu marekani Alfred A.
Montapert. Alfred A. Montapert aliwai kusema “kila binadamu ana uhuru wa
kuchagua,chaguo hilo ndio linaamua matokeo hakuna binadamu aliyewai au
atakayewai kukimbia matokeo ya chaguo alolifanya”.Okwi sawa wanamtaka lakini
nani atoke ili okwi acheze?.Hapo lazima uumize kichwa ili ufanye maamuzi
sahihi.Kwizera na Kiongera wao ndio kwanza walikua wamesajiliwa hawa wawili
wakawa salama.Shida ikabaki kwa Tambwe,Mossoti na Owino.Tambwe kwa upande wake
alikua ametoka kuwa mfungaji bora wa ligi kuu Vodacom msimu ulioisha,hiyo ikawa
pona yake kuenguliwa.wakabaki Owino na Mossoti,Hapa walitumia akili sahihi
ilitumika kumtoa kafara Mussoti na Kumbakiza Owino kwani owino ndio roho ya
beki ya simba.
Tatizo
lililopo Mossoti ni beki na okwi ni mshambuliaji.Ni wachezaji wawili tofauti
uwanjani.Kazi ya Mossoti Okwi hawezi kuifanya na Kazi ya Okwi Mossoti haiwezi.Ilo bado likawa tatizo kubwa
kwa simba.Mpaka sasa wameshacheza mechi 2 na katika hizo mechi 2 wametoa sare
mechi hizo zote mbili.Wamefunga mabao matatu na kufungwa magoli matatu.Na huo
ukawa muda sahihi wa wachambuzi wa mpira Tanzania kuanza kuhoji maamuzi ya simba kumtoa kafara mossoti na
kumrudisha okwi kundini.Ukiangalia mabao mawili waliofungwa simba yalitokana na uzembe wa mabeki.Wachambuzi
wakaanza kuwa na mashaka na kuachwa kwa mossoti,wengi wanaamini makosa
wanayofanya mabeki wa simba angekuepo mossoti yasingefanyika.Nakumbuka mtu
mmoja tukiwa uwanja wa taifa wakati Danny Mrwanda anafunga goli akanifuata na
kuniambia “unaona,simba wameamua kubaki uchi baada ya kuuza suruali waliyokua
nayo na kununua shati”
Lakini
mimi bado naamini viongozi wa simba walisoma vizuri maandishi yaliyoandikwa na
kalamu ya Friedrich Von Wieser kuhusu
kanuni yake ya “Opportunity Cost” .Ukiangalia simba ikicheza bado utaona
ilimuhitaji okwi zaidi ya inavyomuhitaji mossoti.Okwi kwa simba ni kama Messi kwa Barcelona au
Ronaldo kwa Real Madrid.Hakuna goli la simba lililofungwa msimu hii pasipo
msaada wa Emmanuel okwi ila lipo goli simba
wamefungwa hata angekuwepo
Mossoti wangefungwa tu.Okwi ndio moyo wa simba.ndie Mchezaji pekee wa simba
anayeweza kuamua matokeo uwanjani.Wachezaji wa aina ya okwi ndio wale
waingereza wanawaita” Match Winner”.Unafikiri ni timu gani Duniani isiyehitaji
mchezaji anayeamua matokeo?.Unafikiri ibrahimovich atakataa Barcelona
wakimwambia awape Cahil ili yeye apewe messi?.
Kinachowagharimu simba ni kwa mabeki wao
wawili chipukizi mugeveke na
Isihaka kukosa udhoefu wa ligi.Isihaka na Mugeveke ni mabeki wazuri ila
hawajiamini. Wakizoea ligi naamini
watakua miongoni mwa mabeki bora Tanzania na pia wanamsimbazi watamsahau
mossoti.Kwenye swala la kati ya mossoti na okwi nani alikua muhimu msimbazi
bado nipo pamoja na viongozi wa Simba,Hapa nawapa pongezi kwa kutumia vizuri
kanuni ya ”Opportunity cost” ambayo
ilitungwa na hekima ya kalamu ya Friedrich Von Wieser.
No comments:
Post a Comment