ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Monday, January 12, 2015

KOPUNOVIC;SIMBA NI BORA KULIKO YANGA


Baada ya kumzidi mjanja Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm kwa kutinga fainali za michuano ya Kombe la Mapinduzi? Tega sikio.

Baada ya kutinga fainali ya Kombe la Mapinduzi,  Kopunovic amesema hakuwa na hofu kukutana na Yanga SC katika michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya tisa tangu ianzishwe 2007.

Simba imefanikiwa kuifuata Mtibwa Sugar FC fainali baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Zanzabar katika mechi ya pili ya nusu-fainali iliyochezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar jana usiku.

Mara tu baada ya mechi hiyo kumalizika huku kiungo Said Hamis Ndemla wa Simba SC akitangazwa mchezaji bora wa mechi na kukabidhiwa zawadi ya king’amuzi cha Azam FC, Kopunovic alipigwa swali na waandishi kuhusu hofu yake juu ya kasi iliyooneshwa na wapinzani wao wa jadi Yanga SC, lakini Mserbia huyo akasema kamwe hakukihofia kikosi hicho cha Jangwani.

“Ha, ha, haah! Mimi? Niulizeni swali jingine kama lipo. Ningelihofu ningeliambiwa Real Madrid inakuja kushiriki mashindano haya, siyo Yanga. Hiyo Yanga haipo hata fainali kwa sasa. Je, mechi ya fainali haitachezwa kwa sababu Yanga haipo?” Alihoji Kopunovic aliyeiongoza Simba SC katika mechi nne akianza na mechi yao ya pili ya Kundi C waliyoshinda bao 1-0 dhidi ya Mafunzo FC Januari 3.

Kocha huyo hakuwa benchini wakati kikosi cha Msimbazi kikikung’utwa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar FC katika mechi yao ya kwanza ya Kundi C. Kocha huyo alikuwa amekaa Jukwaa la VIP A la Uwanja wa Amaan akiisoma timu ykae hiyo mpya.

Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Polisi Zanzibar, Khamis Sufian alisema alikiandaa kikosi chake kucheza soka la kujilinda weakitarajia matuta lakini kimeangushwa na kipa Mohamed Abdulrahim aliyeshindwa kuokoa shuti la faulo la Ramadhani Singano ‘Messi’ lililokwenda moja kwa moja langoni katika dakika ya 26.

Polisi ilifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuwang’oa kwa matuta waliokuwa mabingwa watetesi KCCA ya Uganda wakati Simba SC iliing’oa Taifa ya Jang’ombe kwa kipigo kibaya cha mabao 4-0 ikiwa ni sawa na kipigo ilichokipokea kutoka kwa Yanga SC katika hatua ya makundi.

No comments:

Post a Comment